Posts

Showing posts from May 6, 2016

LEO KESSY ANATINGA UZI WA YANGA

Image
Kilichobaki kati ya Yanga na beki Hassan Kessy ni kuweka saini kwenye mkataba pekee. Yanga na beki huyo ambaye mkataba wake Simba unakwisha, wamefikia mwafaka baada ya kukubaliana kila kitu na leo matarajio makubwa atasaini rasmi na kuwa mchezaji wa Yanga. Si unakumbuka Kessy aliomba apewe jezi namba 25 iliyokuwa inavaliwa na Emmanuel Okwi. Sasa huenda akakabidhiwa leo rasmi. Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga, zimesema baada ya kuona hana uhakika wa kubaki Msimbazi, Kessy amefanya mazungumzo na uongozi wa Yanga na wamemalizana kwa kuwa mkataba wake Simba, ‘umeisha’. “Nakuambia kila kitu kati ya Yanga na Kessy kimeisha. Suala la kusaini ndiyo lilikuwa halijakamilika, ila Ijumaa, mambo yote yanakamilika na Kessy anasaini kuanza kuichezea Yanga,” kilieleza chanzo. Kessy amekiri kufanya mazungumza na Yanga pia. “Kweli lakini nafikiri meneja wangu ndiye anaweza kulizungumzia hilo,” alisema. Alipotafutwa meneja wake, Tippo Athumani ‘Zizzou’ ambaye ni kiungo wa z

Wabunge wanawake UKAWA watoka nje ya Bunge

Image
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaounda Umoja wa katiba ya wananchi Ukawa wametoka nje ya ukumbi wa Bunge kwa kushinikiza kiti cha spika wa Bunge kuchukua hatua. Akizungumza nje ya ukumbi wa Bunge kwa niaba ya wenzake Mbunge wa Kawe Halima Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) amesema wamekasirishwa na kitendo cha Mbunge wa Ulanga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Goodluck Mlinga ''Wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Katiba na Sheria Mbunge Mlinga alisema kwamba wabunge wa UKAWA hususani Chadema ili waweze kuwa wabunge wa viti maalum ni lazima wawe na mahusino ya kimapenzi na viongozi wao ili waweze kuchaguliwa jambo hilo limetudhalilisha kwa sababu sisi huwa tuna utaratibu wa chama wa kikatiba ambao huwezesha mbunge kuchaguliwa kutokana na uwezo wake wa kisiasa ili aweze kuja kulitumikia taifa''- Amesema Halima Mdee. Mdee ameongeza ku

MAAJABU:Kichwa cha binadamu kuanza kupandikizwa

Image
Mtaalam wa upasuaji wa mfumo wa neva (neurosurgeon) Sergio Canavero kutoka nchini Italia, anakusudia kufanya jaribio la kwanza la kupandikiza kichwa cha binadamu kwenye mwili wa binadamu mwingine, ifikapo mwakani. 3 Wataalam wengi wa upasuaji wanafikiria wazo hilo ni la kiuwendawazimu, lakini sio kwa mtaalamu huyo, kwani anasema bado anapanga kujaribu pandikizo la kwanza la kichwa kwa binaadamu. (Head Transplant) Dk. Canavero ambaye mpaka sasa ameshapata mtu wa kujitolea kufanya zoezi hilo, kijana mwenye asili ya Urusi ambaye ni mtaalam wa software Valery Spiridonov, ambaye ana tatizo la kupoteza nguvu kwa misuli yake ya mwili. Dk. Canavero amesema mafanikio yake yameonesha kuwa mpango wake wa kupandikiza kichwa cha binadamu kwa mwili wa mtoaji (donor) bado upo, na ataanza mpango huo mwishoni mwa mwaka 2017 na unaweza kuwa njia ya kutibu waliopooza mwili. “Ningesema tuna takwimu

MICHEZO:FARIDI MUSA ALASHAVU HISPANIA

Image
Winga wa kimataifa wa Tanzania, Farid Mussa wa klabu ya Azam FC amefaulu majaribio katika klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania.