Posts

Showing posts from April 23, 2016

HABARI MBAYA KWA MASHABIKI WA LIVERPOOL

Image
HABARI MBAYA KWA SAKHO: Beki kisiki wa klabu ya Liverpool Mamadou Sakho amefeli vipimo vya awali vya matumizi ya madawa yasiyotakiwa mchezoni, mchezaji huyo alifanyiwa vipimo hivyo baada ya mchezo wa pili wa ligi ya EUROPA dhidi ya Manchester United. Kwasasa Sakho amesimamishwa na klabu ya Liverpool hivyo hatacheza mchezo wa ligi ya primia dhidi ya Newcastle United akisubiriwa vipimo vya pili vifanyike na kujua hatima yake. Kama matokeo ya vipimo vya pili yatafanana na yale ya kwanza Sakho atafungiwa kucheza soka kwa kipindi kirefu, kama ilivyokuwa kwa beki mwenzake Kolo Toure ambaye alipatikana na hatia ya kutumia madawa yasiyotakiwa na kufungiwa miezi sita. Kwasasa ushiriki wa Liverpool kwenye michuano EUROPA upo salama kwasababu ni mchezaji mmoja tu ndiye ambaye anahusika kwenye uchunguzi, tofauti na ambapo ingekuwa ni wachezaji wawili jambo ambalo lingesababisha klabu kufungiwa kushiriki.

TUPO SAFARINI

Image
Maisha ni safari ndefu sana, hatuna budi kusafiri..... Nami nasema; Uhai ni zawadi asilia, hatuna budi kuuheshimu hata wa wale walio dhaifu. Maisha ni matumaini yanayo waka katika kila moyo, tuyaache yakiwaka. Maisha ni mwanga unao fungua njia mpya, tuyafungue pamoja. Maisha ni kile ambacho sisi sote tunakitamani, shangwe, furaha na haki ya kila mmoja. Maisha ni safari ya pamoja....tusafiri pamoja bila kubaguana

MAANA YA TABASAMU

Image
*Tabasamu ni dirisha linalofunguka kuonesha mwonekano wako wa kwanza mbele za watuTabasamu ni muhimu sana katika maisha kwa sababu kubwa kabisa tatu ambazo ni kama ifuatavyo:* *Kwanza:Tabasamu ndiyo asset kubwa, ujumbe na signal ambazo tabasamu hutoa kwa watu wengine huonesha jinsi tulivyo, nini tunahitaji, na namna na jinsi tulivyo.Tabasamu ni kama kipimo cha nje cha mood na jinsi tunavyoonekana.* *Pili:Tabasamu hueleza haraka na moja kwa moja kama mtu unaingilika (approachable), tabasamu huonesha nini tutataka kwa wengine na pia huonesha kwamba wanathamani.*