Pambano la kufunga mwaka Bondia CHEKA kuzipiga na Dullah Mbabe Jumapili ya Desemba 25
Bondia Dullah Mbabe ameapa kumstaafisha ngumi mpinzani wake Francis Cheka katika pambano lisilokuwa na ubingwa litakalopigwa siku ya Jumapili ya Desemba 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam Bondia Francis Cheka Dullah Mbabe amesema, mazoezi anayoyafanya ya kumjenga pamoja na rekodi yake anaamini atampiga Cheka kwani anaamini hakuna bondia anayeweza kumfikia kwa sasa kwa uwezo na kiwango alichonacho na lengo lake katika pambano hilo ni kumstaafisha Cheka kama alivyofanya kwa Bondia Mada Maugo. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa mabondia hawa kukutana, wakiwa wote wametoka kupoteza michezo yao mwezi hu...