Posts

Showing posts from April 27, 2016

PAPA WEMBA ALIJITABIRIA KIFO

Image
Papa Wemba aliwahi kufanya mahojiano na mwandishi wa habari wa Sauti ya Amerika (VOA) nchini DRC Roger Muntu, ambaye pia alikuwa ni mtu anayefahamiana naye zaidi, na akamueleza kuwa anatamani akifa, afie stejini kwani ndiyo sehemu pekee ambayo hujihisi kama anapaa akiwa anaimba. “Alisema nataka nifie stejini, nataka siku zangu za mwisho ziwe jukwaani, nilipomuuliza kwa nini, alisema kwa sababu ndiyo kila muda ninapokuwa jukwaani nikiimba, nahisi kama ninapaa, hivyo ndoto yake ilikuwa kweli”, alisema Roger Muntu akimueleza Papa Wemba. Papa Wemba alifariki siku ya Tar 24 Aprili 2016, akiwa Abidjan nchini Ivorycoast kwenye tamasha la muziki, ndipo alipoanguka ghafla na kufariki dunia muda mfupi baadaye akikimbizwa hospitali. @EATV

PICHA YA PREZOO KWA DAYNA..ILIVURUGA NDOA YA DAYNA

Image
                                  Akizungumza na Enewz Dayna amesema kuwa alikutana na Prezo kabla ya yeye kuwa star mkoani Morogoro katika show ambayo yeye alimfata A.Y kwaajili ya project yake ya kimuziki. “Wakati nipo nao nikatamani kupiga nao picha ya kumbukumbu ambayo baadae mzazi mwenzangu alivyoiona ilikuja kuleta shida hadi ikapelekea tukakosa maelewano na baadaye tukashindwana”, alisema Dayna. Aidha Dayna akiizungumzia skendo ya yeye kutoka kimapenzi na rapper Roma Mkatoliki ameiambia Enewz kuwa yeye na Roma ni washikaji tuu na ushiriki wake katika harusi ya rapper huyo ni moja ya majukumu ya sehemu ya familia kwani kwa sasa yeye amekuwa ni mmoja wa familia hiyo.  Dayna amesema kuwa alikutana na Prezo kabla ya yeye kuwa star mkoani Morogoro katika show ambayo yeye alimfata A.Y kwaajili ya project ...

Diamond ft papa wembe ..R.I.P

Image
Pale DIAMOND akifanya Colabo na PAPA WEMBA