Posts

Showing posts from January 21, 2017

Jinsi ya kupata hamu ya kula

Image
Mtu anaweza kujikuta akikosa kabisa hamu ya kula kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya, au kuishi na wasiwasi, hofu, mawazo au majonzi. Unapokosa hamu ya kula mara kwa mara huchangia sana mhusika kukonda na kupungua uzito pamoja na kushuka kwa kinga ya mwili hivyo kushambuliwa na maradhi kirahisi zaidi. Hapa ninazo njia za kuepuka tatizo hilo la kukosa hamu ya kula kama ifuatavyo:- Ili kukabiliana na tatizo hilo unaweza kutumia limao au chungwa ambavyo ndani yake kuna vitamin C ambayo huongeza hamu ya kula kwa mhusika, hivyounaweza kula matunda hayo au kutengeneza juisi yake ili kupata msaada zaidi. Pia unaweza kutumia kitunguu swaumu kwani husaidia sana kuamsha mfumo wa chakula na kufanya kazi vizuri na kuongeza hamu ya kula. hata hivyo kitunguu swaumu hicho unaweza kukitafuna au kuunga kwenye chakula. Halikadhalika tangawizi nayo ni msaada mkubwa wa tatizo hili na huleta hamu ya kula kwa wale ambao hukosa kabisa hamu ya kula. Hata hivyo ni vyema ikafahami...