Posts

Showing posts from May 10, 2016

JIONEE SIMU 10 ZA GHARAMA DUNIANI

Image
 #1 – Falcon SuperNova Pink Diamond iPhone 6  ($95.5 Million) (Tsh190,000,000,000)  #2 – iPhone 5 Black Diamond  ($15.3 Million) (Tsh30,600,000,000)  #3 – iPhone 6 Amosu Call Of Diamond  ($2.7 Million) (Tsh5,400,000,000)  #4 – GoldVish Le Million  ($1.3 Million) (Tsh2,600,000,000)  #5 – Diamond Crypto Smartphone  ($1.3 Million) (Tsh2,600,000,000)  #6 – Gresso Luxor Las Vegas Jackpot  ($1 Million) (Tsh2,000,000,000)  #7 – Vertu Signature Cobra  ($310,000) (Tsh620,000,000)  #8 – Black Diamond VIPN Smartphone  ($300,000) (Tsh600,000,000)  #9 – Savelli Smartphone  ($250,000) (Tsh500,000,000) #10 – iPhone Princess Plus  ($170,400) (Tsh340,800,000)

UZIWI UNAWEZA KUTOKEA KWA KUTUMIA SPIKA ZA MASIKIONI

Image
Sauti kutokana na matumizi mabaya ya spika za masikioni ( earphones & headphones ) zaweza kutuweka katika hatari ya kupata uziwi. Katika zama hizi za maendeleo ya digitali, kumekuwepo ongezeko la matumizi la vifaa vya kielektroniki kama rununu, runinga na kompyuta. Matumizi ya vifaa hivi huambatana na spika za mezani pamoja na spika za masikioni ili kumraisishia mtumiaji kusikiliza na kufurahia muziki. Spika za masikioni zimetengenezwa ili kumuwezesha mtumiaji kusikiliza sauti kutoka katika kifaa chake wakati wowote atakapohitaji na hata kama amezungukwa na mazingira yenye kelele. Usikilizaji wa sauti ya juu au sauti kubwa kwa kutumia spika za masikioni kwa muda mrefu kunaweza kupelekea kupata uziwi pia hata uziwi wa moja kwa moja. Usikilizaji huu wa sauti kubwa ni hatari zaidi kwa watoto na vijana kwa kuwa hupendelea kusikiliza muziki kwa sauti ya juu aidha nyumbani au katika vilabu vya muziki, kwenye magari na hata kwa kutumia spika za masikioni. Sauti hupimwa kwa kutu

AFYA; Umuhimu wa mazoezi

Image
  Mwili wa binadamu waweza kufananishwa na nyumba inayojengwa, nyumba hujengwa kwa matofali, simenti, chokaa na malighafi nyingine nyingi, na inahitaji ukarabati wa mara kwa mara ili iendelee kuwa nyumba bora, nyumba iliyoachwa kukaliwa na binadamu huchakaa haraka na pengine hubomoka kabla ya wakati wake. Mwili wa binadamu nao kama ilivyo nyumba una mahitaji yake, unahitaji chakula bora ili uendelee kubaki katika hali ya afya nzuri, pia unahitaji mazoezi ya viungo ili uweze kuwa imara na wenye nguvu. Mwili wa binadamu hata viumbe wengine(wanyama) unapokosa mazoezi hunyong’onyea na mifumo ya mwili hushindwa kufanya kazi vizuri inavyotakiwa. Mazoezi ya mara kwa mara au kufanya kazi zinazohusisha matumizi ya nguvu ya mwili yanasaidia mifumo mingi ya mwili kufanya kazi inavyotakiwa, mazoezi yatatuepusha na magonjwa ya moyo, kisukari, na hata magonjwa mengine hayataweza kushambulia miili yetu, na ni njia nzuri ya kupunguza uzito wa mwili uliozidi. Unapokuwa unafanya mazoezi m

ADHARI ZA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE

Image
   HISIA Miaka ya hivi karibuni imeibuka aina mpya ya kushiriki tendo la ndoa kwa mtindo wa kisasa ambao unahusisha mapenzi kinyume na maumbile. Suala hili linatokana na utandawazi  ambapo wanawake na wanaume  huiga mtindo huo kutoka mataifa ya magharibi  kupitia intaneti pamoja na video za ngono. Aidha wanawake na wanaume huiga staili hiyo ya kushiriki tendo la ndoa pasipo kuogopa madhara ya kiafya  yanayoweza kutokea kwa wanawake na wanaume. Mtindo huo unao onekana kuwa ni wa kisasa  una hatari kubwa kwa afya kati ya mwanaume na mwanamke. Kuiga iga mitindo ya  maisha ya  kimagharibi pasipo kuangalia madhara yake  ni hatari kwani watu wengi waliowahi kuhusika katika mtindo huo wanajutia maamuzi yao kutokana na madhara waliyoyapata. Yafuatayo ni madhara yanayoweza  kutokea kwa upande wa mwanaume: -Kuziba mirija  katika sehemu ya siri ya mwanaume Kwa upande wa mwanamke ni pamoja na Kupanuka na kusababisha kutokwa na haja kubwa katika kipindi mwanamke anapot