MICHEZO: Zlatan kupewa ofa ya mkataba na Man United
Zlatan Ibrahimovic bado hajapokea ofa rasmi ya mkataba kutoka kwa Manchester United, wakala wake amethibitisha usiku wa kuamkia leo. Mapema leo, siku kadhaa kabla ya Ibrahimovic kuichezea Paris Saint Germain mchezo wa mwisho, Radio RMC France imeripoti kwamba United tayari wameshampa mshambuliaji huyo wa Sweden mkataba wa mwaka mmoja. Lakini wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola alionge na Sky Sports News na kukanusha taarifa hizo. “Kwenye dunia ya sasa inabidi tukubaliane na ukweli kwamba kuna baadhi ya waandishi wa habari hutengeneza story – hii sio taarifa ya kweli,” alisema Raiola. RMC Radio ndio kituo cha habari ambacho kwa mara ya kwanza walianza kuripoti usajili wa mshambuliaji Anthony Martial kutoka Monaco kwenda Man United, leo waliripoti kwamba tayari United wamempa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja Zlatan kujiunga nao mara Jose Mourinho atakapopewa timu kuiongoza. Ibrahimovic Alithibitisha Ijumaa iliyopita kwamba angeondoka PSG mwishonu mwa msimu na kuna b...