Posts

Showing posts from May 21, 2016

MAHITAJI SITA YA KIHISIA KWA MWANAUME

Image
1. Kuaminika (Trust) - Mwanaume anahitaji kuaminika. Ni vizuri sana kujua unaaminiwa. Kuhusiana na maamuzi ya kifedha, Maamuzi yanahusiana na malezi, n.k. Kwa mwanaume kuhisi anaaminiwa, Mwanamke anahitajika kuwa mu-wazi na kueleza mahitaji yake pasipo kificho ama hila. Kwa kuwa hili ni jambo la asili kwa mwanamke, mwanamme anatakiwa kuwa makini kwa mwanamke anapokuwa anazungumza. Anapofanya hivyo, hitaji la kwanza la msingi la kihisia la mwanaume linakuwa limetimizwa. Endapo mwanamme anahisi kuwa anaaminiwa, hitaji la mwanamke la kujaliwa nalo linakuwa limetimizwa. 2. Kukubalika (Acceptance) - Wakati unapoweza kwa dhati na kwa uwazi kumpokea mwanaume na "mapungufu yake" yote, anahisi kukubalika. Hili ni la muhimu kwa afya ya hisia za mwanaume katika mahusiano. Mara ya kwanza, unaweza usihisi kama anafanya kile unachotaka afanye ili kukusaidia. Kama utamkubali kwa jinsi alivyo na ukafanya juhudi za kupata msaada zaidi pale ambapo unakuwa unauhitaji, ataj

Mabaki ya ndege ya Misri yapatikana

Image
Jeshi la Misri limepata mabaki ya ndege hiyo kilomita 290 kaskazini ya Cairo. Baadhi ya mizigo ya abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo pia imepatikana. Kinachotafutwa sasa ni kisanduku cha mawasiliano au "black box" Ndege ya Misri. Juhudi za kutafuta kisanduku kinachorekodi mawasiliano au Black box cha ndege hiyo inaendelea. Ndege hiyo ya Misri ilianguka usiku wa kuamkia Alhamisi ikiwa na abiria 66 miongoni mwao wahudumu wa ndege hiyo. Shughuli ya kutafuta mabaki yake ilianza jana na sasa imezaa matunda baada ya kupatikana kwa mabaki ya ndege hiyo kilomita 290 kutoka Cairo pamoja na baadhi ya mizigo ya abiria waliokuwemo ndani yake pia imepatikana. Waziri wa safari za anga nchini Misri amesema uwezekano kuwa ndege hiyo ilishambuliwa kigaidi angani ni mkubwa kuliko hitilafu za mitambo kusababisha kutoweka kwake. Waziri mkuu wa Misri Sherif Ismail alipoulizwa uwezekano wa njama ya kigaidi katika mkasa huo amejibu kuwa hawapuuzilii sababu yoyote ina

Ajali ya meli ya MV Bukoba iliyotokea mwaka 1996 (miaka 20 iliyopita) siku kama ya leo

Image
Siku ya LEO  tarehe 21 Mei ni siku ya kumbukumbu ya ajali ya meli ya MV Bukoba iliyotokea mwaka 1996 (miaka 20 iliyopita) katika Ziwa Victoria. Mabaki ya miili ilizikwa sehemu moja katika eneo la Igoma jijini Mwanza. Kupitia kwa Mwanamitindo wa Kimataifa @FlavianaMatata chini ya ‪#‎ FlavianaMatataFoundation‬ wanafanya semina za Usalama wa vyombo vya majini na kushiriki kwenye misa ya kuwaombea wahanga wa ajali hiyo. Flaviana ni mmoja kati ya watu waliopoteza ndugu (Mama) zao kwenye ajali hiyo na amekuwa akifanya kumbukumbu hii kila mwaka. ‪#‎ MvBukoba20‬ ‪#‎ UsalamaMajini‬