Mfahamu KIM JONG-UN-Rais wa Korea ya Kaskazini
STAAJABIKA NA KIM JONG-UN (ALMAARUFU KWA JINA LA KIDUKU) RAIS WA KOREA KASKAZINI. Kim Jong- un ni mtoto wa tano na wa mwisho katika uzao wa Kim jog-il (raisi wa pili wa Korea Kaskazini). Kwa sasa ndiye kiongozi wa nchi hiyo na alichukua cheo hicho baada ya kifo cha baba yake Dec 19, 2011. Kim jong-un anatajwa kuwa mmoja wa viongozi wenye msimamo mkali hasa kwa nchi za kimagharibi na hadi sasa ameimarisha nguvu za kinyuklia za korea kaskazini na anainyima usingizi Marekani. Hebu sasa tuyajue machache yafuatayo kumuhusu Kim jong-un: 1. Ni general pekee duniani aliyepata cheo hicho bila uzoefu wa kijeshi. Kipaji, akili na kujituma ndo vilimfanya kuwa general licha ya kutokuwa na mafunzo wala uzoefu wowote wa masuala ya kijeshi. Labda ni kwa sababu Kim ni shupavu na jasiri wa kuzaliwa na sio wa kujifunza. Na anapenda zana za kinyuklia kuliko zana nyingne za kijeshi. 2. Pamoja na kuwa kiongozi na mkuu wa nchi, Kim hakusoma shule yoyote nchini Korea kaskazini. Ali...