Posts

Showing posts from December 27, 2016

Mchezaji wa LIVERPOOL -Firmino akamatwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa

Image
Mchezaji wa Liverpool Roberto Firmino ameshtakiwa kwa kosa la kuendesha gari akiwa mlevi baada ya kukamatwa mkesha wa siku ya Krismasi. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alikamatwa baada ya gari lake kusimamishwa katikati mwa Liverpool mapema siku ya Jumamosi ,polisi wamesema. Mchezaji huyo wa Brazil anatarajiwa kufikishwa mbele ya hakimu wa Liverpool mnamo Januari 31. Firmino atawasilishwa mahakamani siku ambayo timu yake itakabiliana na Chelsea katika uwanja wa Anfield. Liverpool ilimsajili mchambuliaji huyo kutoka Hoffenheim kwa kandarasi ya miaka mitano iliogharimu kitita cha pauni milioni 29 mwezi Juni. Alicheza katika ushindi wa wiki iliopita dhidi ya Everton katika uwanja wa Goodison Park. Liverpool imesema kuwa haitazungumzia swala hilo hadi pale hatua hiyo ya kisheria itakapokamilika. @chanzo - bbc swahili

Msichana aliyetengwa kwa kuwa na hedhi afariki

Image
Maafisa wa polisi huko Nepal wanachunguza kifo cha msichana wa miaka 15 aliyefukuzwa hadi katika mtaa wa mabanda kwa kutokwa na hedhi. Wanasema kuwa msichana huyo alikosa hewa na kufariki baada ya kuwasha moto ili kupata joto. Chini ya tamaduni za Hindu kwa jina Chhaupadi, wanawake walio na hedhi ama ambao wamejifungua huonekana kuwa wachafu. Tamaduni hiyo ilipigwa marufuku na serikali ya Napoli mwaka 2005, lakini bado inaendelea kutekelezwa katika maeneo ya mashambani yaliopo magharibi. Image copyright EPA   Mwili wa Roshani Tiruwa ulipatikana na babake wikendi iliopita katika jiwe na nyumba moja ya matope katika kijiji cha Gajra, Wilayani Accham yapata kilomita 440 magharibi mwa Kathmandu. Baadhi ya jamii katika maeneo ya mashambani zinaamini kwamba watakabiliwa na janga baya iwapo wanawake walio katika hedhi hawatatengwa. Hu...