Posts

Showing posts from November 1, 2016

Inashauriwa kukojoa baada ya Tendo la ndoa kufanyika

Image
Mara nyingi tunashauriwa kukojoa kila baada ya tendo la ndoa. Japokuwa wanawake wengi pamoja na kuwa na hamu ya kwenda haja ndogo kila baada ya tendo ila kutokana na uvivu na uchovu ujikuta katika usingizi mzito na kusahau tendo hili muhimu baada ya kufika kileleni. Umuhimu wa tendo hili ni kupunguza na kuzuia uwezekano wa kupata maambukizi ya magonjwa ya njia ya mkojo(U.T.I) na magonjwa ya zinaa(S.T.I) Ikumbukwe kuwa tendo la ndoa huongeza presha kwenye kibofu na kusababisha hamu ya kukojoa kila baada ya tendo hali inayokuwezesha kuondoa vimelea vya magonjwa mbali mbali kabla ya kusambaa kwenye kibofu na sehemu nyingine za mwili kusababisha matatizo makubwa. kwa wanaotumia kondomo pia unashauriwa kufanya hivo endapo itapasuka sambamba na kusafisha sehemu za uke na uume kwa maji safi na sabuni. kwa wanaofanya mapenzi ya mdomo(chumvini na kulamba kone) unashauriwa kutoingiza shahawa, maji maji ya uke/ume na damu mdomoni kwani kuna hatari kubwa ya kuambukizwa magonj

MUHIMU: Njia rahisi ya kuzuia ugonjwa wa U.T.I

Image
Kunywa maji mengi kiasi cha glasi 6 mpaka 8 itakusaidia kukojoa mara kwa mara na hupunguza idadi ya maambukizi katika njia ya mkojo. Epuka vyakula na vinywaji vinavyoweza kukuweka katika hatari ya maambukizi, kama kahawa na pombe ambavyo hupunguza kinga za mwili. Safisha njia ya mkojo(Urethra) kila baada ya kukojoa na kufanya tendo la ndoa kuanzia mbele kuelekea nyuma ili kuepuka wadudu katika njia ya haja kubwa kuingia katika njia ya mkojo Epuka dawa na poda zinazopuliziwa katika njia ya haja ndogo au kuingiza vitu au vidole pasipostahili huweza kuchubua sehemu hizo na kufanya urahisi wa maambukizi. Vaa nguo za ndani asili ya pamba na zisizobana sana kuacha hewa ya kutosha ili kupunguza maambukizi. Usibane mkojo kila unapojisikia kwenda haja fanya hivyo ili kuepuka wadudu kusukumwa na kusambaa katika kibovu na figo. Usilale au kukaa kwa kukunja miguu muda mrefu kwani utawatengenezea mazingira mazuri wadudu ya kuzaliana na kusambaa sehemu za juu za mwi