Msichana aliyetengwa kwa kuwa na hedhi afariki

Maafisa wa polisi huko Nepal wanachunguza kifo cha msichana wa miaka 15 aliyefukuzwa hadi katika mtaa wa mabanda kwa kutokwa na hedhi.
Wanasema kuwa msichana huyo alikosa hewa na kufariki baada ya kuwasha moto ili kupata joto.
Chini ya tamaduni za Hindu kwa jina Chhaupadi, wanawake walio na hedhi ama ambao wamejifungua huonekana kuwa wachafu.
Tamaduni hiyo ilipigwa marufuku na serikali ya Napoli mwaka 2005, lakini bado inaendelea kutekelezwa katika maeneo ya mashambani yaliopo magharibi.
Image copyright EPA 

Mwili wa Roshani Tiruwa ulipatikana na babake wikendi iliopita katika jiwe na nyumba moja ya matope katika kijiji cha Gajra, Wilayani Accham yapata kilomita 440 magharibi mwa Kathmandu.
Baadhi ya jamii katika maeneo ya mashambani zinaamini kwamba watakabiliwa na janga baya iwapo wanawake walio katika hedhi hawatatengwa.
Huku wakiwa wametengwa hunyimwa chakula chao cha kila siku na hawaruhusiwi kunywa maziwa.
#Chanzo BBC Swahili

Popular posts from this blog

SIFA ZA MWANAMKE MNENE KITANDANI NA RAHA YAKE.

mazoezi kwa ajili ya kufanya uke uwe tight(mnato)

Faida ya kula BAMIA -na kazi yake mwilini

KAZI YA SHANGA KIUNONI NA MAANA YA RANGI ZAKE........