Jinsi ya kupata hamu ya kula

Mtu anaweza kujikuta akikosa kabisa hamu ya kula kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya, au kuishi na wasiwasi, hofu, mawazo au majonzi.

Unapokosa hamu ya kula mara kwa mara huchangia sana mhusika kukonda na kupungua uzito pamoja na kushuka kwa kinga ya mwili hivyo kushambuliwa na maradhi kirahisi zaidi.

Hapa ninazo njia za kuepuka tatizo hilo la kukosa hamu ya kula kama ifuatavyo:-

Ili kukabiliana na tatizo hilo unaweza kutumia limao au chungwa ambavyo ndani yake kuna vitamin C ambayo huongeza hamu ya kula kwa mhusika, hivyounaweza kula matunda hayo au kutengeneza juisi yake ili kupata msaada zaidi.

Pia unaweza kutumia kitunguu swaumu kwani husaidia sana kuamsha mfumo wa chakula na kufanya kazi vizuri na kuongeza hamu ya kula. hata hivyo kitunguu swaumu hicho unaweza kukitafuna au kuunga kwenye chakula.

Halikadhalika tangawizi nayo ni msaada mkubwa wa tatizo hili na huleta hamu ya kula kwa wale ambao hukosa kabisa hamu ya kula.

Hata hivyo ni vyema ikafahamika kuwa hili tatizo la kukosa hamu ya kula mara nyingine huwa ni kiashiria tosha kwamba mhusika anadalili za homa au kuna tatizo ndani ya mwili wake hivyo ni vyema kuwaona wataalam wa afya kwa uchunguzi zaidi

Popular posts from this blog

SIFA ZA MWANAMKE MNENE KITANDANI NA RAHA YAKE.

mazoezi kwa ajili ya kufanya uke uwe tight(mnato)

Faida ya kula BAMIA -na kazi yake mwilini

KAZI YA SHANGA KIUNONI NA MAANA YA RANGI ZAKE........