Mfahamu KIM JONG-UN-Rais wa Korea ya Kaskazini



STAAJABIKA NA KIM JONG-UN (ALMAARUFU KWA JINA LA KIDUKU) RAIS WA KOREA KASKAZINI.
Kim Jong- un ni mtoto wa tano na wa mwisho katika uzao wa Kim jog-il (raisi wa pili wa Korea Kaskazini).
Kwa sasa ndiye kiongozi wa nchi hiyo na alichukua cheo hicho baada ya kifo cha baba yake Dec 19, 2011.
Kim jong-un anatajwa kuwa mmoja wa viongozi wenye msimamo mkali hasa kwa nchi za kimagharibi na hadi sasa ameimarisha nguvu za kinyuklia za korea kaskazini na anainyima usingizi Marekani.

Hebu sasa tuyajue machache yafuatayo
kumuhusu Kim jong-un:
1. Ni general pekee duniani aliyepata cheo hicho bila uzoefu wa kijeshi. Kipaji, akili na kujituma ndo vilimfanya kuwa general licha ya kutokuwa na mafunzo wala uzoefu wowote wa masuala ya kijeshi. Labda ni kwa sababu Kim ni shupavu na jasiri wa kuzaliwa na sio wa kujifunza. Na anapenda zana za kinyuklia kuliko zana nyingne za kijeshi.
2. Pamoja na kuwa kiongozi na mkuu wa nchi, Kim hakusoma shule yoyote nchini Korea kaskazini. Alipelekwa kwa siri nchini
Swirtzerland akiwa mdogo na alisoma Bern
international school ya nchini humo. Mkuu wa shule alimtambulisha darasa la sita A kama Park un na kwamba alikuwa mtoto wa mwanadiplomasia wa korea kaskazini (kwa sababu za kiusalama). Somo alilofaulu vizuri ni mziki lakini alifeli hesabu na sayansi.

3. Anaweza kuwa ndo kiongozi mkubwa wa nchi na mwenye umri mdogo zaidi dunian japo haifahamiki ni lini hasa Kim jong-un alizaliwa. Wapo wanaodai alizaliwa mwaka 1982, wengine 1983, na taarifa nyingne zinasema alizaliwa mwaka 1984.
4. Baba yake, aitwae "KIM Jong-IL" alizaliwa kimiujiza. Taarifa nchini korea kaskazin zinasema Kim jong-il alizaliwa mlima Baekdu, Huu ni mlima wa imani na huabudiwa na wakorea kaskazin.
Wakati, saa na siku aliyozaliwa, nyota mpya ilitokea na kufunika mbingu, ghafla majira yalibadilka kutoka winter kwenda spring na pinde mbili za mvua zilionekana. Japo taarifa kutoka katika kumbukumbu za kisoviet zinasema alizaliwa 1941 katika kijiji cha Vyatskoye huko nchini siberia. Huyu ni baba wa kim jong-un.
5. Alikuwa na uwezo wa kubadili
majira na hali ya hewa, hii ni kwa sababu inadaiwa alikuwa mtu wa miujiza.
6. Akiwa na miaka 27 Kim jong-un alifanyiwa plastic surgery ili kuwa na mwonekano sawa na babu yake Kim II sung. Hii ni kwa sababu Wakorea
kaskazin wengi hawamiliki vyombo vya habari na hivyo wengi hawakuwahi kumuona ila siku walipomuona walimfananisha na hayati kim II
sung na kwa hilo wakatokea kumpenda sana kwakuwa alifanana na babu yake ambaye ndo baba wa taifa wa korea kaskazin na kwao huyu ni Mungu wao na wanaamini yupo nao hadi leo Katika maisha yake ya nje ya uhai.
7. Mwaka 2012, wachina walidai Kim jong-un ni "Sexiest man alive" na kwamba jamaa ni ndoto ya kila mwanamke hapa duniani. Hii ni kutokana na mwonekano wake, ushupavu,, ukarimu, kujiamini pamoja na mvuto wa sura yake ya mviringo.
8. Baba yake alipofariki mwaka 2011 alihakikisha msiba wake unaombolezwa na wakorea kaskazini wote. Ambao hawakujua namna ya kulia, alihakikisha wanayatoa machozi. Ambao hawakushiriki kwa namna moja ama nyingne katika shughuli muhimu za msiba huo
yakiwemo mazishi walihukumiwa kufanya kazi ngumu miezi sita.
9. Alimuhukumu kifo kamanda msaidizi wa jeshi la wananchi kwa kosa la kuhudhuria msiba wa baba yake akiwa amelewa. Amri aliyoitoa ni kwamba " anyongwe na usibaki hata unywele wake".
10. Kim jong-un pia alitoa hukumu ya kifo kwa mjomba wake kwa kile kinachodaiwa kuwa kosa la ubadhilifu wa mali ya umma na harakati za kupindua nchi. Huyu alivuliwa nguo na kutupwa katika banda la mbwa wakali waliomzika katika matumbo yao.
11. Mmoja kati ya marafiki wakuba wa kim jong-un ni nyota wa zaman wa NBA Michael Jordan. Akiwa mwanafunzi, kim alitumia muda wake mwingi kuchora picha za Michael Jordan.

Huyo ndo KIM JONG-UN Rais anayewanyima amani korea kusini na mshirika wake Marekani
na anadai yupo tayari kwa lolote dhidi ya
marekani hasa kwa nguvu za kinyuklia.
Anaendeleza kile walichokiamini babu na baba yake kuwa Marekan ndo adui mkubwa wa Korea kaskazini.




Popular posts from this blog

SIFA ZA MWANAMKE MNENE KITANDANI NA RAHA YAKE.

mazoezi kwa ajili ya kufanya uke uwe tight(mnato)

Faida ya kula BAMIA -na kazi yake mwilini

KAZI YA SHANGA KIUNONI NA MAANA YA RANGI ZAKE........