HABARI MBAYA KWA MASHABIKI WA LIVERPOOL
HABARI MBAYA KWA SAKHO:
Beki kisiki wa klabu ya Liverpool Mamadou Sakho amefeli vipimo vya awali vya matumizi ya madawa yasiyotakiwa mchezoni, mchezaji huyo alifanyiwa vipimo hivyo baada ya mchezo wa pili wa ligi ya EUROPA dhidi ya Manchester United.
Kwasasa Sakho amesimamishwa na klabu ya Liverpool hivyo hatacheza mchezo wa ligi ya primia dhidi ya Newcastle United akisubiriwa vipimo vya pili vifanyike na kujua hatima yake.
Kama matokeo ya vipimo vya pili yatafanana na yale ya kwanza Sakho atafungiwa kucheza soka kwa kipindi kirefu, kama ilivyokuwa kwa beki mwenzake Kolo Toure ambaye alipatikana na hatia ya kutumia madawa yasiyotakiwa na kufungiwa miezi sita.
Kwasasa ushiriki wa Liverpool kwenye michuano EUROPA upo salama kwasababu ni mchezaji mmoja tu ndiye ambaye anahusika kwenye uchunguzi, tofauti na ambapo ingekuwa ni wachezaji wawili jambo ambalo lingesababisha klabu kufungiwa kushiriki.