AFYA; ..FAIDA YA JUICE YA MATUNDA MWILINI

Juisi ni kinywaji bora na maarufu duniani, lakini ni vyeme ukajua juisi ipi ina faida mwilini na ipi haina faida yoyote. Katika zama tulizonazo, kumezuka aina nyingi za vinywaji vinavyoitwa juisi, wakati si juisi bali ni vinywaji vyenye ladha ya matunda mbalimbali.
Juisi ni kinywaji kilichotengenezwa kutokana na tunda halisi au mboga na si mchanganyiko wa maji na kemikali nyingine zenye ladha ya matunda na kupewa majina kama juisi ya machungwa, nanasi, zabibu, n.k. Mara nyingi vinywaji hivyo huwekewa sukari na kemikali nyingine za kuhifahdia (preservertives) ili zisiharibike, ambavyo kiafya havikubaliki.
Licha ya kutumia jusi halisi kama kinywaji tu, juisi pia hutoa kinga na tiba kwa maradhi mbalimbali. Iwapo mtu atatengeneza mchanganyiko maalum wa matunda na kutayarisha juisi maalum na kuinywa, anaweza kupata kinga na tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya kama ilivyoanishwa hapa chini:
KAROTI+ KITUNGUU SWAUMU + EPO
Juisi ya mchanganyiko wa karoti, kitunguu swaumu na epo (apple) husafisha sumu mwilini na kuupa mwili 
 nguvu.

EPO+TANGO+FIGILI
Juisi ya mchanganyiko wa tunda la epo, tango na mboga ya majani aina ya Figili (celery) hutoa kinga ya saratani, hupunguza mafuta ya kolestro mwilini na huondoa hali ya kuchafuka kwa tumbo na kuumwa kichwa.
NYANYA+KAROTI+EPO
Juisi ya mchanganyiko wa nyanya, karoti na epo huboresha rangi ya ngozi na huondoa harufu mbaya mdomoni.

CHUNGWA+TANGAWIZI+TANGO
Juisi ya mchanayiko wa machungwa, tangawizi na matango huboresha ngozi na hushusha joto la mwili.
NANASI+EPO+TIKITI MAJI
Juisi ya mchangayiko wa nanasi, epo na tikitimaji huondoa mlundikano wa chumvi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo pamoja na figo. Hii ina maana kwamba juisii hii ni kinga tosha dhidi ya magonjwa ya kibofu cha mkojo na figo.
KAROTI+EPO+PEASI+EMBE
Juisi ya mchangayiko wa karoti, epo, peasi na embe hushusha joto la mwili, huondoa sumu mwilini, hushusha shinikizo la damu na hupambana na matatizo ya kupumua.
PAPAI+NANASI+MAZIWA
Mchanganyiko wa papai, nanasi na maziwa, ambao una kiwango kikubwa cha vitamin C, E na Chuma (Iron), huboresha rangi ya ngozi na kuifanya iwe nyororo na husaidia mmeng’enyo wa chakula tumboni (metabolism).
NDIZI+NANASI+MAZIWA
Nao mchangayiko wa ndizi, nanasi na maziwa una vitamin nyingi na virutubisho vingi na huondoa tatizo la ukosefu wa choo.

Kwa ujumla, juisi ya mchanganyiko wa matunda hayo ukitumiwa kama ipasavyo hutoa kinga tosha dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mwili na huweza pia kuwa tiba ya magonjwa yaliyotajwa hapo awali.

Ili uone faida za matunda katika suala zima la afya ya mwanadamu, jenga mazoe ya kula matunda hayo kabla hujapatwa na maradhi, kwani kwa kufanya hivyo utaupa mwili wako ile kinga yake ya asili ya kupambana na adui maradhi.

SC...DullonetAfya.com

Popular posts from this blog

SIFA ZA MWANAMKE MNENE KITANDANI NA RAHA YAKE.

mazoezi kwa ajili ya kufanya uke uwe tight(mnato)

Faida ya kula BAMIA -na kazi yake mwilini

KAZI YA SHANGA KIUNONI NA MAANA YA RANGI ZAKE........