MAHITAJI SITA YA KIHISIA KWA MWANAUME
1. Kuaminika (Trust) - Mwanaume anahitaji kuaminika. Ni vizuri sana
kujua unaaminiwa. Kuhusiana na maamuzi ya kifedha, Maamuzi yanahusiana
na malezi, n.k. Kwa mwanaume kuhisi anaaminiwa, Mwanamke anahitajika
kuwa mu-wazi na kueleza mahitaji yake pasipo kificho ama hila. Kwa kuwa
hili ni jambo la asili kwa mwanamke, mwanamme anatakiwa kuwa makini kwa
mwanamke anapokuwa anazungumza. Anapofanya hivyo, hitaji la kwanza la
msingi la kihisia la mwanaume linakuwa limetimizwa. Endapo mwanamme
anahisi kuwa anaaminiwa, hitaji la mwanamke la kujaliwa nalo linakuwa
limetimizwa.
2. Kukubalika (Acceptance) - Wakati unapoweza kwa dhati na kwa uwazi
kumpokea mwanaume na "mapungufu yake" yote, anahisi kukubalika. Hili ni
la muhimu kwa afya ya hisia za mwanaume katika mahusiano. Mara ya
kwanza, unaweza usihisi kama anafanya kile unachotaka afanye ili
kukusaidia. Kama utamkubali kwa jinsi alivyo na ukafanya juhudi za
kupata msaada zaidi pale ambapo unakuwa unauhitaji, atajihisi
kukubalika. Mwanaume anapojihisi kukubalika kwa jinsi alivyo, inakuwa ni
rahisi kwake kutimiza mahitaji ya msingi ya mwanamke ya kumwelewa.
3. Kutambulika (Recognition) - Umewahi kusikia msemo "Watoto huililia,
Wanaume huifia". Tunaongelea Kutambulika. Hakuna kilicho kizuri kama
kutambulika kwa kufanya kazi nzuri, hata katika mahusiano yako.
Kutambulika ama kuthaminiwa kwa juhudi zako, hata katika mahusiano yako.
Kutambulika ama kutahaminiwa kwa juhudi zako kwaweza kwenda mbali.
Wakati ambapo wanaume wameweza kutambuliwa mchango wao wanajua kuwa
mchango wao si bure ama kuwa inachukuliwa kirahisi na watakuwa tayari
kuridhisha hisia za tatu za wake zao zinazohusu kuheshimiwa (Respect)
4. Shauku (Admiration) – Kuwa na shauku na mumeo kwa urahisi ni kumuweka
katika viwango vya juu vya kujali na kumfurahia. Mwanamume anapohisi
kuwa anaheshimika kiwango hicho, nguvu zake hujitokeza kwa kung'aa.
Kwamba ni mchekeshaji, Mwenye nguvu, Mkweli, anavutia kimapenzi
(romantic), n.k. Sifa zote hizi zinajitokeza kwa uwazi zaidi pale mke
anapoonesha kuwa na shauku ya mumewe. Mwanaume anapoona shauku hii toka
kwa mkewe, Hitaji la nne la mke la uaminifu (Loyalty) linakuwa
limetimizwa.
5. Kuthibitika (Approval) – Hili ni kubwa lakini pia dogo. Kuthibitika
ni jambo dogo kiasi kwamba kama halikueleweka, laweza kufanya madhara
zaidi kuliko wema. Kwa lugha ya picha, hili ni hitaji la msingi la
mwanamke la kihisia pia isipokuwa kuna tofauti ndogo. badala ya
"kuthibitisha" mwanamke anahitajika kuthaminiwa (Validated). Kwamba
anakubali ama anakataa. Kila mwanamme anapenda kuwa shujaa kwa mkewe.
Hii haimaanishi kuwa lazima ukubaliane na kila kitu anachofanya au
kusema. Kuthibitisha kwako inamaanisha kuwa unamtambua na kuheshimu kwa
mambo mema anayofanya katika mahusiano yenu.
6. Kutia moyo (Encouragement) – Mwanaume anahitaji kutiwa moyo na mkewe.
unapomtia moyo mkewe, inampatia tumaini na ujasiri kukupatia mahitaji
yako yote ya msingi ya hisia za kimahusiano. Wakati ambapo mke
anamuamini, Kumkubali, Kumtambua na kuwa na shauku na mumewe, hili
linamtia hamasa ya kuendelea kutimiza mahitaji yote ya kihisia ya
mwanamke.
@marriage family