UREMBO:Njia tano za kukuza nyewe zako

 
Moja ya imani kubwa iliyojengeka miongoni mwa waafrika hasa watanzania ni kwamaba nywele nyeusi hazikui kwa urahisi kama aina nyingine za nywele kama za wazungu, wahindi na waarabu. Ukweli ni kwamba nywele aina zote zinakuwa kwa wastani wa nusu inchi kwa mwezi anasema DR Del Sandeen mtaalam wa nywele nyeusi. Wanawake wengi wenye nywele nyeusi wamakuwa wakiteseka sana mpaka kufikia hatua ya kuzikata nywele zao au kuvaa nywele za bandia (wigi). Hakuna haja ya kuteseka kwani kinachoitajika ni kufuata njia na mbinu zitakazo kutoa kwenye tataizo hili. Zifuatazo ni njia utakazotumia ili kuzifanya nywele zako ziwe zenye afya ndefu na kuvutia.
1.FUATA KANUNI ZA AFYA/KULA VIZURI
Kabla ya kutibu tatizo kwa nje inatakiwa kulitibu kwa ndani. Ni ukweli kwamba vitu unavyokula, kunywa na jinsi gani unautunza mwili wako vina mchango mkubwa katika ukuaji wa nywele zako. Nywele zina Keratini ambayo ni protini inayotengenezwa na amino acid. Ili nywele mpya ziweze kukua, mwili wako unaitaji uzalishe acid inayoitwa amino acid. Kwa hiyo vyakula vyenye proteini ni muhimu kwa ukuaji wa nywele zako. Akikisha unakula vyakula vyenye protini kwa wingi kama mayai, nyama, maharage, samaki na kadhalika.
 
Unatakiwa ule matunda, mboga za majani, kunywa maji mengi na kufanya mazoezi mara kwa mara. Kwa kuwa nywele zako zinakuwa kutoka katika mwili, unapoutunza mwili wako vizuri, jua kua nywele zako, ngozi na hata kucha zinanufaika pia.
Kula vyakula vyenye vitamin C na mbogamboga kama spinachi. Mwili wako unatumia Vitamin C kutengezeza kitu kinachoitwa kitaalam Collagen, ambacho ni muhimu sana kwa ukuaji wa nywele. Vitamini C pia inasidia kupunguza madini ya chuma amabayo ni kikwazo kwa ukuaji wa nywele.
Utafiti unaonesha kuwa watu wanaokumbwa na tataizo la upungufu wa Vitamini na kutokula au kufuata lishe bora mara nyingi wanapatwa na tatizo la kuwa na nywele kavu na zisizorefuka.
2.TUMIA MAFUTA YA KULAINISHA
Kiasili nywele nyeusi ni kavu sana hivyo basi unashauriwa kutumia mafuta kuzifanya ziwe laini. Hapa namaanisha utumie shampoo au air conditioner zilizotengenezwa kwa ajili ya nywele kavu. Zingatia kuwa sio kila mafuta ni mazuri kwa nywele zako kwa sababu kila aina ya mafuta yanatengenezwa kwa ajili ya aina fulani za nywele. Kwa mfano kuna mafuta kwa ajili ya nywele kavu na pia kuna mafuta kwa ajili ya nywele zenye mafuta. Hapa wanawake wengi wanakumbwa na tatizo hili na kujituta wanapaka mafuta wasiyojua yametengenezwa kwa ajili gani. Usipake mafuta kwa kuwa shostito wako amepaka, bali chunguza nywele zako zipo kwenye kundi gani.
3.PUNGUZA NYWELE ZAKO MARA KWA MARA
Kwa kawaida nywele zinakuwa kutoka kwenye mizizi, nywele zilizoharibika zinazuia ukuaji wa nywele mpya hivyo unashauriwa kuzikata nywele zilizoharika kuruhusu nywele mpya kukua. Unashauriwa kukata nywele zako kila baada ya wiki 6 mpaka 10 kwa wastani wa robo inchi au nusu inchi na sio zaidi. Kama anayekuset na kukutengeneza anasisitiza kukata nywele zako kila unapokwenda saloon jua kuwa nywele zako zinaweza zisiwe kubwa. Cha msingi ni kutafuta mtaalam anayejua ni kiasi gani cha nyele kinatakiwa kupunguzwa na ni kwa mda gani na pia ni vizuri kujifunza jinsi ya kupunguza nywele zako. Kumbuka kuwa ukataji holela wa nywele kunasababisha matatizo ya nywele kukua na kuwa mbaya.
4.TUNZA NYWELE ZAKO KWA UMAKINI
Hii ni pamoja na kupunguza matumizi ya kemikali, kutumia vitu vyenye joto kali(heat treatment) na pia kuosha mara kwa mara. Jaribu kupunguza mitindo yenye joto kali, chagua staili ya nywele ambayao haitengenezi sana joto. Unashauriwa uoshe nywele zako mara tatu kwa wiki na kwa kutumia maji ya moto. Hair messaging inasaidia ukuajia wa nywele kwa sababu inasaidia kuongeza msukumo wa damu na kupeleka virutubisho muhimu kwenye nywele zako.
Usitumie rubberband kufunga nywele zako. Kama unataka kufunga nywele zako na kuzibana kwa nyuma usitumie rababendi au kamaba, badala tumia kibanio. Kibanio kinasidia kuzuia nywele zisijizibe sehemu ya kutokea hivyo kukua kwa urahisi
Usizichanae sana nywele zako. Hakuna haja ya kuzichana nywele mara 100 kila siku kwa sababu ukweli ni kwamba usipozichana mara nyingi ndivyo zitakavyokuwa kwa urahisi. Chana nywele zako zinapokuwa kavu na sio zikiwa na majimaji au unyevunyevu.
5.TUMIA STAILI ZA KUZILINDA NYWELE ZAKO
Ni tataizo kwa watu wengi kuwa pindi nywele zinapokuwa kubwa wanapenda kuziachia ili watu wazione ni kubwa kiasi gani. Pia wanawake wengi wanapenda pia kuziacha zipigwe na upepo. Lakini tambua kuwa kutumia mitindo ya kuzilinda kutakusaiodia kuzibakisha kwenye ukubwa wake. Mitindo ya kuzilinda kutakusaidia kuzuia nywele zako zisigusane na nguo, mito au siti ya gari. Kwa kuzifunika nywele zako kutakusaidia kutunza unyevunyevu wa nyele zako na kuzuia ukavu unaosababisha madhara. Funika nywele zako hasa wakati wa kulala.
 

Popular posts from this blog

SIFA ZA MWANAMKE MNENE KITANDANI NA RAHA YAKE.

mazoezi kwa ajili ya kufanya uke uwe tight(mnato)

Faida ya kula BAMIA -na kazi yake mwilini

KAZI YA SHANGA KIUNONI NA MAANA YA RANGI ZAKE........