UZIWI UNAWEZA KUTOKEA KWA KUTUMIA SPIKA ZA MASIKIONI
Sauti kutokana na matumizi mabaya ya spika za masikioni (earphones & headphones) zaweza kutuweka katika hatari ya kupata uziwi. Katika zama hizi za maendeleo ya digitali, kumekuwepo ongezeko la matumizi la vifaa vya kielektroniki kama rununu, runinga na kompyuta. Matumizi ya vifaa hivi huambatana na spika za mezani pamoja na spika za masikioni ili kumraisishia mtumiaji kusikiliza na kufurahia muziki. Spika za masikioni zimetengenezwa ili kumuwezesha mtumiaji kusikiliza sauti kutoka katika kifaa chake wakati wowote atakapohitaji na hata kama amezungukwa na mazingira yenye
kelele.
Usikilizaji wa sauti ya juu au
sauti kubwa kwa kutumia spika za masikioni kwa muda mrefu kunaweza kupelekea
kupata uziwi pia hata uziwi wa moja kwa moja. Usikilizaji huu wa sauti kubwa ni
hatari zaidi kwa watoto na vijana kwa kuwa hupendelea kusikiliza muziki kwa sauti ya
juu aidha nyumbani au katika vilabu vya muziki, kwenye magari na hata kwa kutumia spika za
masikioni. Sauti hupimwa kwa kutumia skeli ijulikanayo kama decibel (dB).Mfano mtu anayeongea kwa
sauti ya chini ni kadirio la 30 dB.
Kwa mujibu wa shirika la afya
duniani (WHO), kupitia takwimu zilizopatikana katika nchi zenye kipato cha kati
zinaonyesha kuwa, miongoni mwa wale walio na umri kati ya miaka 13-35,karibu
asilimia 50 husikiliza sauti katika kiwango kisicho salama kwa kutumia vifaa
vyao binafsi vya sauti na asilimia 40 huwa katika kiwango kisicho salama cha
sauti wakiwa katika kumbi za starehe. Shirika la afya (WHO) limeainisha kuwa,
kukaa eneo lenye kiwango cha sauti kuanzia 85dB kwa masaa nane au 100dB kwa
dakika 15 kuwa siyo salama. Inakadiriwa kuwa 1.1bilioni ya walio chini ya miaka
ishirini(teenagers) na vijana wako katika
hatari ya kupoteza usikivu kutokana na matumizi ya vifaa vya sauti zikiwemo
simu za mkononi(smartphones)
zinazoambatana na spika za masikioni.
Kusikiliza isivyo salama itategemea kiwango cha sauti, muda ambao utasikiliza na ni mara ngapi
unasikiliza.
Inashauriwa kuwa kiwango cha juu
cha sauti katika maeneo ya kazi ni 85dB na isizidi masaa nane kwa siku.
Wafanyakazi wa vilabu vya usiku na baa mara nyingi huwa katika kiwango cha juu
cha sauti na wanashauriwa kupunguza masaa ya kazi. Kwa mfano katika klabu za
usiku, huwa na kiwango cha 100dB kwa hiyo itakuwa salama kwa masikio yetu
endapo tutakaa katika kumbi hizo kwa dakika 15 tu.
souce