DAWA YA MAUMIVU MAKALI YA MAGOTI/ MATATIZO YA MIFUPA

MAUMIVU MAKALI YA MAGOTI/ MATATIZO YA MIFUPA ?(OSTEOPOROSIS)
Huu ni ugonjwa ambao hutokea ambapo uimara wa mifupa unapopungua hivyo kuwa na asilimia uwezrkano mkubwa wa kuweza kupatampasuko au kuvunjika kwa urahisi na mara nyingi ugonjwa huu huambatana na maumivu makali ya mifupa. Ugonjwa huu unaweza kutokea iwapo kutakuwa na mabadiliko ya hormoni,upungufu wa madini kama calicium au vitamin D.
Mifupa ina madini ambayo hutumika mwilini na kurejeshwa ili kuufanya mfupa uweimara na kuujenga, endapo yatatumika zaidi kuliko kurejeshwa katika mifupa,mifupa hudhoofu na hukosa uimara na hupunguza uzito.(normal peak bone mass is greater than normal bone loss)
Uzito wa mfupa kwa kawaida kwa mtu kijana huwa ni 2.5 standard deviations uzito chini ya huo mtu anaweza kupata (Osteoporosis) tatizo la mifupa. Utajua uzito huo kwa vipimo maalumu yani kwa dual energy X-ray
absorptiometry.
Mara nyingi tatizo hili la mifupa hutokea katika uti wa mgongo (huweza kusababisha mgongo kupinda na kuuma), hutokea katika Magoti,katika nyonga na kifuani.
VITU VINAVYOWEZA KUSABABISHA MATATIZO YA MIFUPA (OSTEOPOROSIS)
-Upungufu wa hormone za Estrogen hii huwapata sana wenye menopause.
-Ulevi
-Upasuaji wa kuondolewa ovaries
-Magonjwa ya figo
-(Hyperthyroidism) tatizo la utengenezwaji wa thyroid homoni nyingi kipita kiasi na hivyo kusababisha mwili usifanye kazi vizuri
-(Anorexia)uzito Mdogo kupita kiasi unao sababishwa na tabia ya kujinyima kula kupita kiasi,kufanya mazoezi kupita kiasi kwa kuogopa kunenepa au kutaka mtu abaki akiwa na kilo chache sana ukilinganisha na urefu wake.
-baadhi ya matibabu,madawa yenye kemikali(chemotherapy) kama steroids,proton pump inhibitor na anti seizure medications
-Uvutaji wa sigara
-kutokufanya mazoezi ya viungo vya mwili
KINGA ZA MATATIZO YA MIFUPA (OSTEOPOROSIS)
~Zingatia ulaji mzuri hasa utotoni
~Epuka matibabu yenye kutumia kemikali
~Pendelea ulaji mzuri wa vyakula vya asili vyenye madini yakutosha na muhimu yanayo jenga mifupa
~acha au punguza matumizi ya pombe
~Fanya mazoezi ya kutosha na kunywa maji mengi ya kutosha
MADHARA YANAYOWEZA KUSABABISHWA NA TATIZO HILI
Maumivu makali ya mifupa katika Magoti,uti wa Mgongo,mabegani,kifuani au katika nyonga
~Kupinda Mgongo hasa wakati wa uzeeni
~Kuvunjika mifupa kwa urahisi
MATIBABU YA OSTEOPOROSIS
~Kula kwa wingi chakula chenye kiasi kikubwa cha vitamins D na chenye madini ya calcium mfano maziwa,ubuyu,moringa Oleifera leaves n.k
~Tumia Dawa asili zinazofanya homoni za estrogens kuwa sawia(kwa wanawake)
~Tumia Dawa zitakazo saidia kukupatia madini ya calicium ya kutosha na itakayo weza kuimarisha mifupa.
~Mafuta ya samaki na samaki wa maji baridi kwa wingi upate fatty acid.
~Mafuta ya nazi nimazuri kwa mifupa.

Source @KHALID GUGU 

Popular posts from this blog

SIFA ZA MWANAMKE MNENE KITANDANI NA RAHA YAKE.

mazoezi kwa ajili ya kufanya uke uwe tight(mnato)

Faida ya kula BAMIA -na kazi yake mwilini

KAZI YA SHANGA KIUNONI NA MAANA YA RANGI ZAKE........