Satelaiti ya Facebook ya kufikisha mtandao kasi Afrika yaharibiwa





 Mwanzilishi wa kampuni ya Facebook Mark Zuckerberg amelezea kusikitishwa kwake baada ya satelaiti ambayo Facebook ingeitumia kwa mawasiliano ya kasi ya mtandao wa intaneti barani Afrika kuharibiwa.
Satelaiti hiyo iliharibiwa katika mlipuko uliotokea eneo la Cape Canaveral jimbo la Florida, Marekani siku ya Alhamisi.
Satelaiti hiyo kwa jina Amos-Six ilikuwa imebebwa na roketi ya Falcon Nine ambayo ililipuka ilipokuwa ikifanyiwa majaribio ya kujiandaa kwa safari ya siku ya Jumamosi.
Mlipuko huo ulitokea wakati roketi hiyo ilikuwa ikijazwa mafuta na kutikiza majengo yaliyokuwa umbali wa kilomita kadha.
Bw Zuckerberg, ambaye yumo ziarani Afrika, amesema "nimesikitishwa sana" kusikia kwamba satelaiti hiyo iliharibiwa.
"Tutaendelea kujitolea katika lengo lengo la kufikisha huduma ya mtandao kwa kila mtu na tutatia bidii hadi kila mtu apate nafasi na manufaa ambayo yangetokana na satelaiti hii," aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

 
 
Image captinRoketi ya Falcon 9 ilipolipuka
Hakuna aliyejeruhiwa wakati wa mkasa huo.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa kulipuka kwa roketi hiyo ni pigo kubwa kwa mwanabiashara Elon Musk ambaye ni mmiliki wa kampuni ya kuunda roketi ya Space X.
Afisa mmoja wa masuala ya anga za juu wa Israeli amesema satelaiti ya Amos-6 inakadiriwa kuwa na thamani ya $200m (£150m) na ilimilikiwa na kampuni kwa jina Spacecom, was a major blow to the industry.
"Hili ni pigo kubwa sana ambalo huenda ikaathiri mustakabali wa sekta ya satelaiti na huenda ikahitaji kupigwa jeki (kifedha)," alisema mwenyekiti wa taasisi ya masuala ya anga za juu ya Israel, Isaac Ben-Israel.

@CHANZO BBC

Popular posts from this blog

SIFA ZA MWANAMKE MNENE KITANDANI NA RAHA YAKE.

mazoezi kwa ajili ya kufanya uke uwe tight(mnato)

Faida ya kula BAMIA -na kazi yake mwilini

KAZI YA SHANGA KIUNONI NA MAANA YA RANGI ZAKE........