JINSI YA KUPIKA TAMBI ZA MAYAI



 JINSI YA KUPIKA TAMBI ZA MAYAI


MAHITAJI

Tambi 1/2 paket
Vitunguu maji 2 vikubwa
Karoti 1
pilipili hoho 1
Vitunguu swaumu kijiko 1 cha chakula
Carry powder kijiko 1 cha chai
Njegere zilizo chemshwa 1/2 kikombe
Mafuta ya kupikia kiasi
Chumvi kwa ladha upendayo
mayai 2

MAANDALIZI

1: Chemsha maji yachemke sana, weka chumvi na mafuta kiasi, weka tambi katika maji yaliyo chemka ziache ziive kiasi; sikiisha iva chuja maji na uziache kavu.
2: Chukua bakuli gonga  mayai kisha weka pembeni.
3: Chukua kikaango kilicho safi weka jikoni tia mafuta kiasi na utaendelelea kuweka vitunguu maji,vitunguu swaumu,hoho ,karoti na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo mdogo na havitakiwi kuiva sana.
4: kisha tia tambi na njegere katika mchanganyiko wako na uendelee kukaanga kwa dakika kadhaa.
5: chukua mayai tia katika tambi ongeza moto kiasi, ili tambi zako zichambuke ,moto hautakiwi kuwa mdogo sana ikiwa moto ni mdogo tambi zako zitashikana na kutia mabonge , mayai ya kiiva hapo chakula chako kitakuwa tayari kwa kuliwa



Popular posts from this blog

SIFA ZA MWANAMKE MNENE KITANDANI NA RAHA YAKE.

mazoezi kwa ajili ya kufanya uke uwe tight(mnato)

Faida ya kula BAMIA -na kazi yake mwilini

KAZI YA SHANGA KIUNONI NA MAANA YA RANGI ZAKE........